Jaji Abraham Mwampashi:aamuru kesi ya Uamsho kupelekwa Mahakama kuu

Monday, 11 March 20130 comments


uamsho

Kufuatia kesi inayowakabili Viongozi wa Jumuia ya Uamsho na mihadhata ya Kiislamu Zanzibar ya kusababisha kutokea matendo bali mbali ya uharibu wa mali ya umma na uchafuzi wa amani Nchini imesikilizwa tena leo hii.
Kama kawaida vingozi hao walifikishwa Mahakamani Vuga  mnamo majira ya saa mbili asubuhi wakiwa chini ya ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi na takribani maeneo yote yanayoizungumka Mahakama hio yalilindwa na vikosi vya  jeshi la JKU na baadhi ya askari Polisi wengine kwa lengo la kuimarisha usalama zaidi Mahakamani hapo.
Kama kawaida yao jopo la mawakili la watuhumiwa hao hao likiongozwa na Salum Taufik na wenzake wanaowatetea viongozi hao waliendelea tena kulalamikia suala la kupatiwa dhamana kwa wateja wao  huku  wakisema kua kuwanyima dhamani kwa wateja wao sio haki kishria.
Nae Jaji Abraham Mwampashi ambae amesikiliza kesi hio amesema kua kitendo kilichofanywa na DPP cha kuzuia dhamana kwa viongozi hao  sio sahihi  na ni kuingilia Mahakama katika utendaji wa kazi zake  hivo basi maamuzi yote ya DPP kuwanyima dhamana hayakuwa sahihi kisheria  na amewataka Mawakili hao kufungua kesi Ndani ya Mahakama kuu ambayo itakuwa na uwezo wa kutolea maamuzi ya dhamana kwa wateja wao.
Aidha Jaji huyo aliendelea kusema kua hata hivyo  pingamizi lenyewe la kuwanyima dhamana  viongozi hao halikuwa halali na halikufuata taratibu zilizostahiki ambazo zimewanyima dhamana viongozi hao, kwani pingamizi hizo hazikusikilizwa na Mahakama husika ambayo ndio walipaswa kuzuia dhamana hio na badala yake maamuzi hayo ya kunyimwa dhamana yalitolewa na Mrajisi kwa maagizo ya dpp ambae hakuwa na  Mamlaka ya kufanya hivo kisheria.
Pia amefahamisha kuwa Maamuzi ya kuwanyima dhamana  Mashehe hao hayakuwa sahihi kwani Mrajisi hakuwa na Mamlaka ya kusikiliza Shitaka linalowakabili viongozi hao  badala yake  lilipaswa kusikilizwa Mahakama husika ambayo ni Mahakama kuu na ndio iliyokuwa na uwezo wa kutoa maamuzi kama ni yakuwanyima dhamana au kupewa dhamana.
Sambamba na hayo kutokana na Jaji huyo kutokuridhika na mwenendo mzima wa kesi hio ameamua kufuta maamuzi ya mrajisi na ameamuru kuw kesi hio kwa sasa isikilizwe Mahakama kuu ambayo ndio yenye uwezo wa kusikiliza kesi hio na kuitolea uamuzi sahihi unaofaa.
Hata hivyo jopo hilo la Mawakili limendelea tena kuihoji Mahakama’’ inawezekana mtu akaandika kimemo tu kuzuia dhamana hivi Mahakama inakuwa na kazi gaini hadi inaingiliwa kiasi hicho’’walisema mawakili hao.
Kesi hio inayowakabili viongozi kadaa wa Jumuia hio akiwemo Sheikh Faridi Hadi na wenzake imepangwa kusikilizwa tena siku ya tarehe 26 mwezi huu na watuhumiwa hao kurudishwa tena rumande hadi siku hio itakapotajwa tena kesi yao.
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Zanzibar News - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger