skip to main |
skip to sidebar
Tume ya utangazaji Z'bar (ZBC) yatoa onyo kali kwa Radio Noor
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi-cgqVgBiRznfWF_T72T7cQ617ZR55ctmriKI446KVLKYyFu14pI4A-xGja2Ukn5U7wmNjwjaoL1bGiia_0tvLsSzoYLspnv4RFdzO-FLGZwl8jiaofGLlHYvDR_6kXVZJ4BMW-TOJ6CMA/s320/chande.JPG)
TUME
YA UTANGAZAJI ZANZIBAR (ZBC) IMETOA ONYO KALI KWA IDHAA YAKIISLAM YA
RADIO NOOR FM KUHUSU VIPINDI VYAKE ILIVYOVIRUSHA HEWANI KATI YA TAREHE
17 HADI 19 OKTOBA MWAKA JANA.
KWA MUJIBU WA BARUA
ILIYOWASILISHWA LEO KATIKA STUDIO ZA RADIO NOOR FM NAKUSANIWA NA KATIBU
MTENDAJI WA TUME YA UTANGAZAJI ZANZIBAR TUME HIYO IMEDAI KUWA KWA
MAKSUDI KITUO HIKI KIMEHUSIKA KATIKA KUWASHAJIHISHA WASKILIZAJI
KUSHIRIKI NAKUJIHUSISHA KATIKA VITENDO VYA UVUNJAJI WA AMANI MIKUSANYIKO
PAMOJA NA GHASIA KINYUME NA MAADILI YA KHABARI KAMA INAVYOELEZWA NA
TUME YA UTANGAZAJI ZANZIBAR KATIKA SERA NA MASHARTI YA LESENI YA
UTANGAZAJI.
...
KWA MUJIBU WA BARUA ALIYOPELEKEWA MKURUGENZI WA RADIO NOOR FM YENYE
KUMBUKUMBU NAMBA TUZ/RAN.4/VOL1/22 YA TAREHE 6 MWEZI WA TATU 2013 RADIO
NOOR IMEONYWA KUACHA TABIA HIYO MARA MOJA NA KWAMBA TUME HIYO ITACHUKUWA
HATUA YAKINIDHAMU IWAPO KITUO HIKI KITAREJEA KITENDO HICHO.
HATA HIVYO TUME HIYO HAIKUFAFANUA KUHUSU VIPINDI HIVYO VYA TAREHE 17-19 OKTOBA MWAKA JANA.
AKITHIBITISHA KUPOKEA BARUA HIYO MKURUGENZI WA RADIO NOOR FM AL-USTADH
MOHD SULEIMAN ALI AMESEMA KUWA UONGOZI WA KITUO HIKI UTAKAA NAKUTAFAKARI
KUHUSU ONYO HILO.
AMEFAFANUA KUWA HAONI KUWA WAKATI HUU NI
MUAFAKA KUZUNGUMZIA LOLOTE IWAPO TUME IMEJITOSHELEZA NA UTAFITI WAKE
ILIYOFANYA HAPO AWALI KWA KUTOA DODOSO AMBAZO WALIPEWA BAADHI YA
WASKILIZAJI KUTOA MAONI YAO IWAPO KITUO HIKI KIMECHANGIA KATIKA
KUCHOCHEA VURUGU.
AIDHA MKURUGENZI HUYO AMESEMA KUWA TAARIFA KAMILI ITATOLEWA NA UONGOZI WA RADIO NOOR FM MARA BAADA YAKUITAFAKARI BARUA HIYO.
HIVI KARIBUNI IDHAA NYENGINE YA KIISLAM YA RADIO IMAAN FM INAYORUSHA
MATANGAZO YAKE KUTOKA MJINI MOROGORO TANZANIA BARA ILIFUNGIWA KWA MUDA
WA MIEZI SITA NA KAMATI YA MAADILI YA MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
TCRA KUTOKANA NA MADAI YA KUWASHAJIHISHA WANANCHI WATOSHIRIKI KATIKA
SENSA YA WATU NA MAKAZI.
Post a Comment