Ushiriki wa wajumbe katika vikao vya chama kikamilifu ni muhimu kwa maendeleo ya kuimarisha na kuboresha uhai wa chama.
Wito huo
umetolewa leo na katibu mkuu wa chama cha wananchi cuf ambae pia ni
Makamo wa kwanza wa Rais wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar katika
mkutano mkuu wa wilaya uliofanyika katika ukumbi wa jamat-hani Zanzibar.Katika mkutano huo Maalim Seif amewataka wajumbe hasa hasa wa ngazi za chini kuwa makini na kutilia umuhimu vikao vya chama kwani vikao ndio vinavyotoa maamuzi yaliyo sahihi sambamba na kuonesha uhai wa chama.
Aidha
amewata wajumbe kuhakikisha wanawafuatilia wanachama kulipia ada,
pamoja na kushiriki katika harakati za kisiasa ikiwa ni pamoja na
kuimarisha mikusanyiko ya pamoja kupeana taarifa mbali mbali kuhusu
zinazoendelea Nchini.
Pia
Maalim Seif amefahamisha kuwa harakati za uchaguzi wa ndani ya chama
zinakaribia hivyo amewataka wanachama kujitokeza kugombania nafasi hizo
pamoja na kuwakemea baadhi ya viongozi wa cuf ambao wanalengo la
kuwagawa wanachama kwa ajili ya maslahi yao binafsi.
Aidha ametowa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika ushiriki wa kujiandikisha katika vitambulisho vya taifa sambamba na kuhakikisha wanapata kadi zao za ukaazi.
Amewataka
wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kuhakikisha wanawapata
wale ambao wanasababisha matokeo ya hujma nchini sambamba na serikali
kutoa taarifa ilioyo bayana kwa wananchi.
Post a Comment