Mkurugenzi wa Utumishi na Uendeshaji katika Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar, Rajab Uweje Yakub, alibainisha hayo jijini Dar es Salaam jana katika ziara ya wajumbe wa Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi wa Barabara ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Yakub ambaye alimwakilisha Katibu wa wizara hiyo, Juma Malick, alisema serikali inafanya hivyo kwa kuwa mapato yake ni kidogo, hivyo mapato hayo husaidia kupunguza ugumu wa kuendesha serikali.
Hata hivyo alisema wapo katika mazungumzo kuona ni jinsi gani tozo hiyo inayokusanywa nusu yake ipelekwe kwenye Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA), kwa ajili ya kufidia gharama za udhibiti.
Awali, Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Fadhil Manungi, alisema kuanzia Julai mwaka 2008, SMZ iliamua kuchukua fedha zote zinazotozwa kwa abiria wanaoruka kutoka viwanja vya Unguja na Pemba kwa maelezo kuwa hilo si tozo lililobainishwa kwenye tozo za Muungano.
“Mamlaka imewasilisha ombi lake kwa SMZ Septemba 2009 kuomba ipatiwe mgawo wa angalau asilimia 50 ya makusanyo haya, kama ilivyo kwa idara nyingine za Muungano ili kufidia gharama za udhibiti ambapo kuna pengo kubwa kutokana na udogo wa sekta na mishahara ya soko ya wataalamu.
“Hadi sasa bado hatujajibiwa. Pamoja na hali hii, mamlaka inaendelea kutoa huduma kwenye viwanja vya Unguja na Pemba pamoja na tozo hii kuchukuliwa,” alisema Manungi.
Aliongeza kuwa pia SMZ haiipi mamlaka sehemu ya ada ya utuaji, lakini kwa Bara Mamlaka ya Viwanja vya Ndege inalipia huduma hizi kwa asilimia 30 ya tozo ya utuaji.
Post a Comment