Tamim awataka wana CUF kutokumfata Hamad Rashid

Wednesday, 13 March 20130 comments


Chama cha Wananchi CUF kimewataka wanachama wake huko kisiwani Pemba kuendeleza umoja na mshikamo walionao ili waweze kuifanya Zanzibar kuwa na mamlaka kamili.
Hayo yamesemwa na Tamim Omari Tamim ambae alikuwa miongoni mwa wanachaama ADC kwa sasa  amejiunga na CUF  wakati alipokuwa akiwahutubia Wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo huko viwanja vya Masota Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Tamim amewataka Wananchama wa CUF kisiwani humo wasije wakajaribu kabisa kumfuata  Hamad Rashia kwani kufanya hivo kutakuwa ni sawa na watu waliojisaliti wenyewe.

'Watu walikufa kwa ajili ya chama hiki leo uhame kwa hadaa ya kibwetere huyu Hamad Rashid  musijaribu ndugu zangu, sisi tumemjua dhamira yake ndio maana tuka toka' alisema Tamim

Nae Makamo Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Tifa Machano Khamis Ali amewataka wafuasi wa chama hicho kuhakikisha wanakuwa wa mwanzo kujitokeza katika kuandikisha Vitambulisho vya Taifa muda ukifika.

Kwani kufanya hivo kutaweza kukifanya Chama hicho kushinda katika uchaguzi unaofata “kama tunavojua  CCM wananjama nyingi wanaweza kusema mtu asiekuwa na kitambulisho  asipige kura katika uchaguzi unaofata’’alisema Machano.

Chama hicho bado kinaendelea na mikutano yake ya uimarishaji wa Chama ambapo kwa siku ya kesho kitafanya mkutano wa hadhara huko katika kijiji cha Tumbe Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba mnamo majira ya saa nane mchan.
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Zanzibar News - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger