Kamishna Mussa:waliokamatwa na Silaha ni wahusika wa matukio ya kijambaza Z’bar

Tuesday, 16 April 20130 comments


chap

Jeshi la Polisi Zanzibar limefanikiwa kuwakamata watu wawili ambao wanasadikiwa kuwa ni mjambazi,waliokamatwa  wakiwa na silaha ya SMG yenye risasi 29 ndani yake.
.
Akizungumza na waandishi wa habari huko Ofisini kwake makao makuu ya Jeshi la Polisi Zanzibar ziwani,Kamishna Mussa Ali Musaa aliwataja watu hao ambao ni Faustine Geogre miaka 36 Msukuma wa geita Ushirombo na Mohamed Ali Salum wa Bambuu Bububu.

Alisema kuwa awali Jeshi lake lilifanikiwa kumkamata Faustine wakati akiwa kwenye sehemu za starehe(baaar ya chuo cha mafunzo)ambae walimfanyia mahojiano na badae kumpekuwa na kumkuta akiwa na fedha za kigeni  Dola za kimarekani 100,Naira za Nigeria 3540 na T,shs,370,000/=  pamoja na simu 3 aina mbali mbali.

Kutokana na hatuwa hio ndipo Jeshi hilo badae likaamua kufanya upekuzi nyumbani kwa mtuhumiwa  huyo na kumkuta na vitu vyengine kadhaa vikiwemo’’jeki 1 bisbisi 2 koleo la kukatia nyaya na baadhi ya vitu vyengine kadhaa”alisema kamishna Mussa.

Aidha kamishna huyo alifahamisha kuwa kutokana na kumuhoji mtuhumiwa huyo kuhusu Bunduki anayotumia katika shughuli zake za ujambazi alisema kuwa bunduki anayotumia na baadhi ya vitu vyengine vilivoibiwa viko nyumbani kwa Mohamed Ali Salum wa Bububu ndipo jeshi hilo likaweza kumkata mtuhumiwa huyo mnamo tarehe 12/4/2013 saa nne usiku akiwa nyumbani kwake Bububu.


 Akibainisha baadhi ya vitu vyengine ambavo vimekutwa ndani ya duka kuwa ni  kamishna amesema kuwa ni glove pia moja soksi za kuvalia kichawi nyeusi na kisu kikubwa,pamoja na vitu kadhaa vikiwemo laptop na baadhi ya vitu vyengine ambavyo vikasadikiwa kuwa vimeibiwa.


Sambamba na hayo kamishna Mussa amesema kuwa Jeshi lake litaendelea na  Operesheni ya namna hii za kuwasaka wahalifu kama kawaida ili kuhakikisha uhalisu unatoweka Nchini kwetu,pia ametowa wito kwa wananchi wote waendelee kutoa taarifa kwa Jeshi hilo ili kukomeza uhalifu unaondelea siku hadi siku.
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Zanzibar News - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger