Mkurugenzi wa habari uenezi na mawasiliano ya Umma wa Chama cha Wananchi CUF Mh Salim Bimani amaewataka Wanachama wa CCM pamoja na wa CUF kuacha kabisa itikadi za vyama vyao kwa sasa badala yake waungane kuitete Zanzibar mpaka iwe na mamlaka kamili kitaifa na kimataifa.
Mh: Bimani ameyasema hayo huko Mwambe Mkoa wa Kusini Pemba wakati alipokuwa akizungumza na na Viongozi mbali mbali wa chama hicho kufuatia mwendelezo wa ziara yake ya kuimarisha chama kisiwani humo.
Bimani amewataka Wananchama hao kwa umoja wao wachanae na sera za vyama vyao badala yake kwa sasa ni kushirikiana bila ya kujali itikadi za vyama walivyonavyo mpaka wahakikishe wanaifanya Zanzibar kuwa Nchi kamili na yenye mamlaka ya kuamua jambo wanalolitaka bila ya kuingiliwa kama ilivo hivi sasa.
Sambamba na hayo amefahamisha kuwa kutokana na hatua iliofikia Nchi yetu kwa sasa hapakuwa na haja ya Wananchi kufata sera ya vyama vyao bali walitakiwa wawe na umoja pia waungane wote kwa pamoja ili wainusuru Zanzibar ili isimalizwe kabisa.
Hivo basi amewataka Wananchi hao kuachana na sera za vyama vyao kwa sasa na wala “sera hizo zisiwe ni vikwaz vya kuwafanya wazanzibar kutokudai Nchi yao”.
Aidha amewataka wazanzibar wote kuwa na umoja na mshikamano wa hali ya juu pamoja na kuhakikisha kuwa wanashiriki katika mabaraza ya katiba ili wakayasimamie vyema madai ya wazanzibar walio wengi ya kutaka Zanzibar yenye mamlaka kamili kitaifa na kimataifa.
Ziara hio inatarajiwa kumalizika siku ya tarehe 16 mwezi huu.
Post a Comment