![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgiL9T15C9NcTcqu4beuniFnMm0W7TsT89BVl3enExs4Xyuk7qeT3flYw2LHN3oapQfqyn5e3WaK88m4RdVkmjgI1pp1XyutgNHsFiujlq-4H9AtyZhFMJtbCHCKfAT_0D4uMoyZTJYVpVU/s320/maalim.jpg)
Katibu mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Mh, Maalim Seif Sharif Hamad amemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt, Emmanuel Nchimbi kujiuzulu katika wadhifa wake kutokana na kushindwa kuisimamia Wizara yake katika utekelezaji wa majukumu yanayohusika na wizara hio.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa Chama hicho uliofanyika katika viwanja vya Mbagala Zakhiem Maalim Seif ambae pia ni Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amesema Dkt, Nchimbi analazimika kujiuzulu kutokana na wizara yake kushindwa kusimamia ulinzi wa Wananchi na mali zao.
Mh,Hamad amesema kua suala la ulinzi wa raia na mali zao ni jukumu la serikali hivyo kupitia Wizara ya mambo ya ndani ya Nchi ambayo ndio yenye jukumu la kusimamia ulinzi imeshindwa kutekeleza wajibu huo na hatimae kumekuwa kukibuka kwa vitenddo mbali mbali vya kihalifu vinavyo hatarisha usalama wa Wananchi na mali zao.
Amesema matukio ya kihalifu yanayo endelea kujitokeza Nchini iwemo kushambuliwa pamoja na kuuwawa kwa viongozi na raia wasio na hatia kunatokana na serikali kushindwa kuimarisha ulinzi kwa raia wake.
Kumekuwa na matukio mbalimbali ya kihalifu yanayotokea hapa nchini ambayo wziri Nchimbi na wizara yake wamwshindwa kuyatafutia ufumbuzi hadi leo hivyo hana budi kujiuuzulu kwani ameshindwa kutekeleza wajibu wake kamawaziri anaehusikannaulinzi” alisema Maalim Seif.
Akizungumzia matukio ya kushambuliwa kwa viongozi wa dini yaliotokea Zanzibar hiivi karibuni hayapaswi kuhusishwa na itikadi za kidini kutokana na utamaduni wa muda mrefu wa kuvumiliana kidini uliojengeka kwa Wananchi wa Zanzibar.
Aidha Maalim seif amechukizwa na kauli ya Dkt. Nchimbi kulihusisha tukio la kuuwawa kwa Padre Evarist Mushi na matukio ya kigaidi na kusema ttukio hilo si la kigaidi kwani Zanzibar hakuna ugaidi.
Huyu ana lengo gani na Zanzibar hata kutangaza ugaidi kwa Zanzibar kwani Zanzibar hakuna ugaidi na wala hautatokea kamwe” alisema Maalim Seif.
Akizungumzia mwenendo wa Serikal;I ya Umoja wa kitaifa ya Zanzibar amesema Serikali kwa kiasi kikubwa imefanikiwa kuleta maendeleo kwa Wananchi wake ikiwa ni pamoja kuinua juhudi za wakulima katika ukuzaji wa kilimo chenye tija kwa wakulima na taifa kwa ujumla.
Amesema kuwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyo chini ya mfumo wa umoja kitaifa imefanikiwa kuinua zao la karafuu kwa kupandisha bei ya karafuu kutoka shilingi elfu tatu kwa kilo hadi elfu kumi bei ambayo inampa mkulima asilimia thamanini ya bein ya soko la dunia.
Pia imefanikiwa kukuza kilimo cha mpunga kwa kuwapatia wakulima wa kilimo hicho kwa kuwapatia wataalamu wa kutosha pamoja na kushusha gharama za pembejeo za kilimo ikiwemo mbolea na dawa za kuulia wadudu ili kuwawezesha wakulima kulima kilimo chenye tija na kuondokana na utegemezi wa chakula kutoka nje.
Aidha amesema kuwa serikali imefanikiwa kuongeza kiwango cha mishahara ya wafanyakazi hadi asilimia ishirini na tano kwa wafanyakazi wa kima chachini ili kuweza kujikimu klimaisha.
Nae Naibu katibu mkuu wa CUF Tanzania Bara Mh, Julius Mtatiro amewataka wanachama hicho kujitokeza katika kuwania nafasi za ujumbe wa mabaraza ya katiba ili kuweza kupata katiba bora itakayo endana na mahitaji ya Wananchi.
Amesema kuwa kutokushiriki katika mabaraza ya katiba ya wilaya kutawapa nafasi watu wasiotaka maslahi mazuri kwa wananchi kuingia katika mabaraza hayo jambo litakalo sababisha kukosekana kwa katiba bora.
Mapema Mbunge mstaafu wa nafasi za wanawake wa Chama cha CUF Bi, Hania Chaurembo amewataka akina mama wa Chama hicho kujitokeza kwa wingi katika kugombea nafasi za uongozi katika Chama ili kupata viongozi watakao kiongoza Chama hicho katika kupata ushindi katika uchaguzi mkuu uja wa mwaka 2015.
Post a Comment