Jeshi la Polisi Z'bar lamtia mbaronikwa madawa ya kulevya

Monday, 18 March 20130 comments



Jeshi la Polisi Zanzibar limefanikiwa kumtia mbaroni kijana mmoja raia wa Ugiriki akiwa na madawa ya kulevya takribani kilo tano mpaka sita unaosadikiwa kua ni kokeni.

kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Kamishna wa Jeshi hilo Zanzibar Bwana Mussa Ali Mussa amesema kuwa kijana huyo anajulikana kwa jina la Alex Vasilias Nitis ...mwenye umri wa miaka 24 na ni raia wa Ugiriki na pasport no,13424772 iliyotolewa Nchini Ugiriki.

Aidha kamishna huyo amefahamisha kuwa kitendo chakufanikiwa kumkamata kijana huyo kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa Zanzibar ambapo alikua anapita transit na badae kwenda Italy kumekuja baada ya Jeshi hilo kupata mashirikiano mazuri na wenzao wa Daresalam pamoja na Interpol na ndipo wakafanikisha hatua hio.

''Tumemkamata kijana huyo akiwa na Madawa ya kulevya ndani ya begi lake jeusi ambalo juu yake aliweka kahawa pamoja na viksi ili kuzuia Mbwa maalumu wasiweze kugundua kilichomo ndani''alisema kamishna Mussa.

Sambamba na hayo amefahamisha kua kijana huyo kwa mujibu wa maelezo yake aliotowa kwa jeshi hilo ni kwamba Mama yake ni Mtanzania na Baba yake ni Mzungu ambae anaishi Nchini Ugiriki.

Pamoja na hayo jeshi hilo limefanikiwa kukamata simu mbili ambazo alikua anatumia kijana huyo na inaonekana kuwa kijana huyo alikuwa anafanya mawasiliano nazo na baadhi ya watu hapa Zanzibar, na hadi sasa jeshi hilo linafanya upepelezi wa kina kujua watu hao ni kina nani ili nawao wakamatwe na kufikiswa katika vyombo vya sheria.

Licha ya kukamatwa kwa kijana huyo lakini Kamishna Mussa ametowa wito kwa Jamii kwa ujumla kuwa washirikiane na Jeshi hilo kuwafichua wale wote wanaohusika na madawa ya kulevya kwani tokea mwezi januari mwaka huu hadi sasa Jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata watu sita wakihusika na madawa ya kulevya hapa Nchini.
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Zanzibar News - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger